Kiswahili

Kufikia akili. Kubadilisha maisha.

NeuroReach Africa ni mpango wa wataalamu wa fani mbalimbali na jamii, unaotumia teknolojia na jamii kupunguza pengo la matibabu ya kifafa barani Afrika, tukianzia Kenya na Zimbabwe.

Ukurasa huu una muhtasari wa taarifa muhimu kwa Kiswahili. Kurasa nyingine bado ziko kwa Kiingereza. Read in English

Huduma ya kwanza ya kifafa

Stay. Safe. Side. Saidia.

Stay — Kaa naye

Kaa na mtu huyo. Angalia saa kifafa kinapoanza.

Safe — Salama

Weka mazingira salama. Ondoa vitu vigumu au vyenye ncha kali, na weka kitu laini chini ya kichwa.

Side — Ubavu

Mlaze kwa ubavu taratibu baada ya kutetemeka kukoma, ili njia ya hewa ibaki wazi.

Saidia — Omba msaada

Pata msaada wa matibabu kama kifafa kinadumu zaidi ya dakika tano au kinajirudia.

Usiweke kijiko wala kitu chochote mdomoni mwa mtu anayepata kifafa.

Vitabu vya watoto

NeuroReach Friends Series

Vitabu vyetu vinawasaidia watoto kuelewa kifafa, kupinga unyanyapaa na kuchagua urafiki. The Day the Purple Kite Flew na My Friend Amani vinapatikana kwa Kiswahili, Kiingereza na Kishona. Nchini Kenya kila kitabu ni KSh 550.

Angalia vitabu
Changia

Weka kitabu katika maktaba ya shule

Vitabu 5 kwa shule ndogo (KSh 2,750) au vitabu 10 kwa shule kubwa (KSh 5,500). Unaweza pia kuchangia utafiti wetu na programu za jamii.